Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Idadi ya visa vya kipindupindu Tanzania yazidi kupanda

Idadi ya visa vya kipindupindu Tanzania yazidi kupanda

Serikali ya Tanzania imetoa taarifa kwa Shirika la Afya Duniani (WHO) kuhusu kuongezeka kwa visa vya kipindupindu nchini humo. Kisa cha kwanza kiliripotiwa mnamo mwezi Julai 2015 nchini Tanzania, na aina mpya ya kirusi kungundulika jijini Dar-es-Salaam tarehe 25 Agosti.

WHO inasema, ripoti ya hivi karibuni inaonyesha kipindupindu kimesambaa katika mikoa 13 nchini Tanzania na sasa kimefika kisiwani Zanzibar. Christian Lindenmeyer ni msemaji wa WHO mjini Geneva.

(Sauti ya Christian)

“Tuna visa 4,324 vya kipindupindu, vikiwemo vifo 67 na hii pia imeathiri Zanzibar ambako visa 106 vimeripotiwa”

WHO inasema, kipindupindu kimeathiri pia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo(DRC) ambapo visa zaidi ya elfu tatu vimeripotiwa pamoja na vifo 91.