Ustawi wa wanawake waimarika, changamoto ubaguzi wa kijinsia:Ripoti

Ustawi wa wanawake waimarika, changamoto ubaguzi wa kijinsia:Ripoti

Ikiwa leo ni siku ya takwimu duniani, takwimu mpya katika ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa kuhusu wanawake imesema ustawi wa mwanamke katika miongo miwili iliyopita unazidi kuimarika sanjari na umri wake wa kuishi.

Mathalani ripoti hiyo ya sita kuchapishwa, inasema wastani wa umri wa mwanamke kuishi ni miaka 72 ikilinganishwa na 68 ya mwanaume lakini bado changamoto zinasalia ikiwemo ubaguzi wa kijinsia, ukatili dhidi ya wanawake na mizozo inayosababisha kaya nyingi zaidi kuwa na mzazi mmoja wa kike.

Akizungumza na waandishi wa habari, Lenni Montiel Naibu msaidizi wa Katibu Mkuu Idara ya maendeleo ya uchumi iliyoandaa ripoti hiyo amesema..

(Sauti ya Lenni)

 "Naamini chapisho hilo limekuja wakati muafaka. Kuendelea usawa wa kijinsia na uwezeshaji wanawake vinaendelea kupatiwa kipaumbele kisera duniani kama ilivyodhihirishwa na kutengwa lengo maalum la kuendeleza usawa wa jinsia na malengo endelevu yaliyopitishwa na Umoja wa Mataifa mwezi septemba huko New York.