UNICEF na wadau waleta nuru kwa wazazi wenye VVU Tanzania

UNICEF na wadau waleta nuru kwa wazazi wenye VVU Tanzania

Lengo namba Tatu la malengo ya maendeleo endelevu. SDGs yaliyopitishwa hivi karibuni na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa linagusia ustawi wa afya kwa watu wote bila kujali umri, jinsia na hali yoyote aliyonayo.

Mwelekeo wa kufanikisha afya hiyo hata kwa watu wanaoishi an virusi vya Ukimwi unatia moyo kutokana na huduma zinazoendelea kutolewa kwa wajawazito wanaoishi na VVU.

Wajawazito sasa wanapatiwa huduma za kuepusha maambukizi kwenda kwa mtoto aliye tumboni na hilo limedhihirika nchini Tanzania katika mradi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF kwa ushirikiano na shirika lisilo la kiserikali la kuhudumia wenye virusi vya Ukimwi. PASADA. Je nini kimefanyika? Abdullahi Boru anatanabaisha katika makala hii.