Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Serikali sikilizeni sauti za vijana: Ban

Serikali sikilizeni sauti za vijana: Ban

Serikali ambazo zinafumbia masikio sauti za vijana, zinaporomoka! Amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon wakati akitoa mhadhara kwenye chuo kikuu cha Comenius, kilichopo mji mkuu wa Slovakia, Bratislava.

Ban amesema kusikiliza sauti za vijana ni muhimu wakati huu ambapo idadi yao duniani ni Bilioni Moja nukta Nane, idadi ambayo ni kubwa zaidi kuwahi kufikiwa duniani.

Kwa mantiki hiyo amesihi serikali kuwezesha vijana ili waweze kuchangia katika amani na vijana wapaze sauti zao kwa maslahi ya jamii zao.

Ametolea mfano vijana wanaosomea diplomasia, akisema wanaweza kutumia uwezo wao kujenga daraja la amani kwa maslahi ya taifa na dunia kwa ujumla.

Akiwa chuo hapo, Ban alipokea shahada ya heshima ya Falsafa sambamba na medali ya dhahabu ambapo amesema ameipokea kwa niaba ya Umoja wa Mataifa.