Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kay apongeza kuanza mchakato wa mashauriano jumuishi kuhusu uchaguzi Somalia

Kay apongeza kuanza mchakato wa mashauriano jumuishi kuhusu uchaguzi Somalia

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu kuhusu Somalia, Nicholas Kay, amepongeza kuanza kwa mchakato wa mashauriano jumuishi kuhusu uchaguzi wa mwaka 2016 nchini Somalia.

Bwana Kay amesema hayo wakati akihutubia kikao cha ufunguzi wa jukwaa la mashauriano ya kitaifa, ambako ametoa wito kwa Wasomali kushauriana kwa upana kuhusu mchakato huo wa uchaguzi, kwa moyo wa maafikiano na maridhiano.

Amesema jukwaa hilo ni fursa ya WaSomali kuuonyesha ulimwengu kuwa wapo mbioni kutimiza ahadi ya kuheshimu katiba ya kitaifa ya muda, na kufanya uchaguzi mnamo mwaka 2016.

Aidha, amekaribisha kushiriki kwa mamlaka za mpito za mikoa na majimbo, pamoja na asasi za kiraia katika kongamano hilo, na kuwakumbusha washiriki wote kuhusu wajibu wao katika majuma na miezi ijayo.