Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Guinea Bissau hali ya haki ni ya kutisha, lakini kuna dalili ya kutia moyo, " Mtaalamu wa UM

Guinea Bissau hali ya haki ni ya kutisha, lakini kuna dalili ya kutia moyo, " Mtaalamu wa UM

Mtaalamu Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu uhuru wa majaji na wanasheria, Mónica Pinto, amehimiza serikali ya Guinea Bissau kusaidia na kuipa heshima kazi ya majaji na waendesha mashitaka, ikiwa ni pamoja na kutambua jukumu kubwa la wanasheria  katika mfumo wa mahakama, zoezi hilo la  demokrasia na uimarishaji wa utawala wa kisheria.

Akizungumza baada ya kukamilisha ziara yake rasmi nchini Guinea Bissau, Bi Pinto amesema, mamlaka ni lazima ipe kipaumbele hatua za haraka za kuhakikisha upatikanaji wa haki sawa na kujenga upya uaminifu wa wananchi katika taasisi.

Wakati wa ziara hiyo, Bi Pinto amesema alijoonea utendaji mbaya mkubwa wa kazi katika mfumo wa haki na mapungufu vitu vinavyochangia ukwepaji wa sheria, kutokuwa huru mahakamani na ulaji rushwa.