Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Libya shime undeni serikali: Baraza la usalama

Libya shime undeni serikali: Baraza la usalama

Wajumbe wa baraza la usalama wamerejea tamko lao la  mnamo Oktoba tisa mwaka huu , ambapo walipongeza washiriki  katika majadiliano ya Libya kwa kukamilisha makubaliano ya kisiasa kwa ajili ya serikali ya kitaifa,  baada ya mashauriano muhimu na ya kina yaliyowezeshwa na Umoja wa Mataifa kupitia mwakilishi wake maalum Bernardino León.

Wajumbe wa baraza la usalama wamewataka pande zote nchini Libya kupitisha na kuweka saini makubaliano ya kisiasa kama yalivyowasilishwa Oktoba nane na kufanya kazi pasina shaka katika muundo wa serikali ya makubaliano ya kitaifa.

Wamesisitiza kuwa makubaliano yanatoa matarajio halisi katika kusuluhisha mgogoro wa kisiasa, kiusalama na kikatiba nchini humo.

Wajumbe wa baraza kadhalika wamenukuu azimio la Libya kuhusu vikwazo na kusema kamati ya vikwazo vya nchi hiyo inajiandaa kuwachukulia hatua wale ambao wanatishia amani ya Libya, utulivu na usalama au kudharau mafanikio ya mchakato wa mpito wa kisiasa.