Wakimbizi, msikate tamaa: Ban

17 Oktoba 2015

Akiwa ziarani nchini Italia, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekutana na wakimbizi na kuzungumza nao kwa hisia kali kutoka moyoni huku akiwapa ujumbe wa matumaini.

Takribani watu milioni 60 kote duniani kote wamepoteza makazi kutokana na mizozo na ukosefu wa usalama na wengi wao wamewasili kusaka hifadhi barani Ulaya.

Baada ya kukutana na wakimbizi hao katikati ya mji mkuu wa Italia Roma, Ban kwa hisia amezungumzia sintofahamu ya wakimbizi wanaokimbia machafuko kutoka Mashariki ya Kati na Afrika

Hata hivyo amesema ametiwa moyo na simulizi zao na kwa kundi la watoto aliokutana nao amewaambia

(SAUTI BAN)

‘‘Msipoteze matumaini, msikate tama.’’

Ban amekariri wito wake kwa viongozi wa dunia kuonyesha mshikamano wa kimataifa na huruma kuhusu suala la wahamiaji.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud