Mtoto wa kike, sauti yake yapazwa

Mtoto wa kike, sauti yake yapazwa

Watoto wa kike wanapaswa kupewa fursa wanayostahili ili wawe  viongozi, wafanyabiashara na raia wa siku za usoni, ni kauli ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon, wakati wa maaadhimisho ya siku ya kimataifa ya mtoto wa kike Oktoba 11.

Kwenye ujumbe wake kwa siku hiyo Katibu Mkuu amesema ili kuwezesha watoto wa kike ni lazima kuwasaidia kuepukana na ndoa na mimba za utotoni, ukeketaji, na vile vile kuwapatia elimu bora na kuhakikisha wanakuwa na afya nzuri na ujuzi kuhusu haki zao katika maswala ya afya ya uzazi.

Maadhimisho hayo ambayo yamefanyika katika maeneo mbalimbali duniani, yamewaleta pamoja wadau wa haki za watoto wa kike, wakiwamo watoto wa kike wenyewe ili kupaza sauti juu ya haki, ndoto na ustawi wao. Miongoni mwa nchi zilizoadhimisha ni Tanzania ambapo shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu UNFPA limeratibu. Tuungane na Joseph Msami