Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jumuiya ya kimataifa isiisahau Somalia: UNHCR

Jumuiya ya kimataifa isiisahau Somalia: UNHCR

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbzi UNHCR, limesema juhudi za kusaidia watu wa Somalia kujenga upya nchi yao zinahitajika, hususani kutoka jumuiya ya kimataifa.

Kati ya wakimbizi milioni moja kutoka Somalia, takribani 5,000 wamerejea nchini mwao mwezi Disemba 2014, licha ya ukosefu wa usalama na matarajio, imesema UNHCR.

Shirika hilo limesema lina matumaini kuwa kiasi cha dola milioni 500 chaweza kupatikana wakati wa mkutano wa kuchangisha fedha mjini Brussels Ubelgiji juma lijalo. Adrian Edwards mi msemaji wa UNHCR.

(SAUTI)

"Mkutano wa wiki ijayo ni ya kupata fedha muhimu kwa msaada wa  kuboresha hali ndani ya Somalia. Uboreshaji wa Shule muhimu, fursa ya ajira na mambo mengine. Kwa hiyo, hatua hizi za awali zinatokea wakati kurudi nchini inaweza kuwa na faida zaidi , na watu wengi zaidi watashawishiwa kuamini hii kama fursa ya kweli."