Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Majanga ya kibinadamu duniani, muarobaini ni mshikamano wa kimataifa

Majanga ya kibinadamu duniani, muarobaini ni mshikamano wa kimataifa

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Jan Elliason amesema dunia inakabiliwa na majanga ya kibinadamu makubwa yasiyodhibitika.

Akizungumza kwenye kikao cha mashauriano kuelekea mkutano wa dunia wa masuala ya kibinadamu utakaofanyika Istanbul, Elliason ametoa picha kamili ya hali halisi ya mahitaji ya kibinadamu akisema, watu milioni mia moja wana mahitaji ya haraka ya kibinadamu, huku watu wasiopungua milioni 60 wamefurushwa makwao au kukimbia nchi zao.

Hata hivyo, Elliason amesema..

(Sauti ya Eliasson)

“Japo Idadi ya watu wanaoteseka ni ya juu zaidi, ni vyema kukumbuka kuwa watu hao sio takwimu, bali ni  wanaume, wanawake na watoto wanaoteseka mno, na kwamba kila mkimbizi anastahili awe salama, na kila mhamiaji ana haki na anastahili heshima.”

Halikadhalika, Elliason amesema, hakuna mtu anayetakiwa kuishi na vurugu, ubaguzi au unyanyasaji wa haki zake za kibinadamu.

Kama hatua ya kukabiliana na hali hiyo, Naibu Katibu Mkuu amesema changamoto hizo zinahitaji mshikamano wa kimataifa.