Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuelekea uchaguzi Afrika, komesheni mauaji ya albino: Mtaalamu

Kuelekea uchaguzi Afrika, komesheni mauaji ya albino: Mtaalamu

Kuelekea uchaguzi katika nchi kadhaa za bara la Afrika kumechochea ongezeko la mahitaji ya viungo vya watu wenye ulemavu kwa imani za kishirikika, amesema mtaalamu huru wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Ikponwosa Ero.

Bi. Ero ambaye mwenyewe ni mlevamu wa ngozi amesema katika taarifa yake kuwa serikali zichukue hatua za dharura kulinda kundi hilo, akisihi pia vyama vya siasa vihakikishe wagombea au hata wafuasi wao hawahusiki kwa njia moja au nyingine katika ukiukwaji huo mkubwa wa haki za binadamu.

Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo mauaji ya Albino yamekuwa yakiripotiwa na Balozi Tuvako Manongi, mwakilishi wa kudumu wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa anafunguka.

(Sauti ya Manongi)

Tangu Bi. Ero ashike wadhifa huo tarehe Mosi Agosti mwaka huu, mashambulizi dhidi ya albino yameripotiwa katika nchi Sita ikiwemo Kenya ambako mtu mwenye miaka 56 alishabmuliwa na viuongo vyake kukatwa.