Ban alaani mauaji ya raia 9 na polisi 2 Burundi

Ban alaani mauaji ya raia 9 na polisi 2 Burundi

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moonm amelaani kuuawa kwa raia tisa na poilisi wawili mjini Bujumbura, Burundi mnamo Oktoba 13, 2015, kufuatia ufyatulianaji risasi katika mitaa kadhaa mjini humo.Taarifa kamili na Assumpta Massoi.

(Taarifa ya Assumpta)

Imeripotiwa kuwa raia waliouawa, akiwemo mfanyakazi wa Shirika la Kimataifa la Uhamiaji, IOM, Evariste Mbonihankuye, walipigwa risasi kwa karibu.

Ban ametuma rambirambi zake kwa familia za wahanga, na kutoa wito kwa mamlaka za Burundi zifanye hima uchunguzi wa kina katika mazingira na kiini cha uhalifu huo, ili kuhakikisha kuwa walioutekeleza wanafikishwa mbele ya mkono wa sheria.