Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kutopatikana huduma za kujisafi kunaweza kuhatarisha ajenda mpya ya maendeleo- UNICEF

Kutopatikana huduma za kujisafi kunaweza kuhatarisha ajenda mpya ya maendeleo- UNICEF

Kiwango cha kunawa mikono kwa sabuni kipo chini sana katika nchi nyingi, licha ya faida zake zilizothibitishwa kwa afya ya watoto. Hayo ni kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF, katika kuadhimisha siku ya kimataifa kunawa mikono.

Siku hii, ambayo inaadhimishwa kwa mara ya nane tangu kuasisiwa, inakuja siku chache tu baada ya Umoja wa Mataifa kupitisha Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDGs, yakiwemo kujisafi kwa mara ya kwanza kabisa katika ajenda ya kimataifa.

Moja wa malengo madogo ya SDG ni kufikia upatikanaji wa huduma tosha na sawa za kujisafi na usafi ifikapo mwaka 2030.

UNICEF imesema kuboresha usafi ni lazima kuende sanjari na upatikanaji wa maji na huduma za kujisafi, au la sivyo, watoto wataendelea kuwa wahanga wa magonjwa ambayo yanazuiliwa kwa urahisi, kama vile kuhara.