Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Amani na uwezeshaji kiuchumi vitainua wanawake: Pindi Chana

Amani na uwezeshaji kiuchumi vitainua wanawake: Pindi Chana

Ulinzi kwa wanawake na uwezeshaji kuchumi ni muhimu katika ustawi wa wanawake amesema Naibu waziri wa  maendeleo ya jamii, jinsia na watoto wa Tanzania Pindi Chana katika mahojiano na Joseph Msami wa idhaa ya Kiswahili ya redio ya Umoja wa Mataifa  muda mfupi baada ya kuhutubia kikao cha baraza la usalama kilichojadili azimio namba 1325 kuhusu amani, usalama wa wanawake.

Chana amesema Tanzania imefanya mambo mengi katika kukabiliana na ukatili dhidi ya wanawake na uwekezaji kwenye elimu. Kwanza anaaza kwa kueleza  fursa zilizopo katika kutekeleza azimio hilo.

(SAUTI MAHOJIANO)