Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tanzania na harakati dhidi ya mauaji ya Albino: Balozi Manongi

Tanzania na harakati dhidi ya mauaji ya Albino: Balozi Manongi

Leo katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Tuvako Manongi amezungumza na waandishi wa habari kuhusu hali ya mauaji ya albino nchini Tanzania na kile ambacho kinafanyika kuondokana na vitendo hivyo ambavyo ameviita ni janga. Assumpta Massoi wa Idhaa ya Kiswahili ya Radio ya Umoja wa Mataifa alizungumza na Balozi Manongi kuhusu hali ilivyo na kwanza alianza kwa kugusia filamu iitwayo A Boy from Geita itakayoonyeshwa kwenye Umoja wa Mataifa siku ya Alhamisi.