Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tanzania na hatua za kutokomeza mauaji ya Albino

Tanzania na hatua za kutokomeza mauaji ya Albino

Wakati kamishna wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa, Zeid Ra’ad Al Hussein akisema watu wenye ulemavu wa ngozi, wana haki ya kuishi huru bila ubaguzi na hofu yoyote, Tanzania imesema inaendelea kuchukua hatua kutokomeza mauaji ya albino. Amina Hassan na taarifa zaidi.

(Sauti ya Amina)

Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Tuvako Manongi katika mahojiano na idhaa hii amekiri kuwa mauaji ya albino nchini mwake ni janga lakini..

(Sauti ya Tuvako-1)

Akigusia filamu iitwayo The Boy from Geita itakayoonyeshwa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa kesho,. Balozi Manongi amesema..

(Sauti ya Tuvako-2)

Alipozungumza na waandishi wa habari jijini New York, Marekani, Balozi Manongi amesema janga la mauaji ya albino ni la kila mtu uwe Umoja wa Mataifa, serikali ya Tanzania na hata mashirika yasiyo ya kiserikali yanayopigania maslahi ya kundi hilo hivyo ubia wa dhati ni muhimu badala ya kunyoosheana vidole.