Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatufanyi lipaswalo kusaidia Afghanistan: Ging

Hatufanyi lipaswalo kusaidia Afghanistan: Ging

Mkurugenzi wa operesheni kwenye ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na usaidizi wa kibinadamu,OCHA, John Ging, amesema hali ya kibinadamu nchini Afghanistan licha ya kuangaziwa kwa kina bado usaidizi wake haujatosheleza.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini New York, Marekani, Bwana Ging ambaye alikuwa ziarani Afghanistan na Pakistani  hivi karibuni ametaja sababu ya kutotosheleza kuwa ni mwingiliano wa majanga ya kiasili kama vile mafuriko na yale yanayosababishwa na binadamu.

Amesema mwaka huu pekee watu 130,000 wamepoteza makazi yao kutokana na mizozo ilhali nchi hiyo inahifadhi wakimbizi 300,000 kutoka Pakistani.

Bwana Ging amesema mahitaji yanaongezeka lakini usaidizi wa kifedha kwa ajili misaada ya kibinadamu umepungua kwa karibu asilimia Hamsini kutoka dola Milioni 500 mwaka 2010 hadi dola Milioni 204 mwaka huu, ikimaanisha kwamba..

(sauti ya Ging)

“Ina maana kwamba hatufanyi vitu vyote ambavyo tunapaswa kufanywa wakati ambapo hali ya kibinadamu inazidi kudorora.”