Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ulinzi wa kijamii unasaidia kupunguza umasikini: FAO

Ulinzi wa kijamii unasaidia kupunguza umasikini: FAO

Chapisho jipya la shirika la chakula na kilimo FAO linaonyesha kuwa mikakati ya ulinzi wa kijamii kama vile uhamishaji wa fedha tasilimu, chakula mashuleni na kazi za kijamii inasaidia kiuchumi hususani kwa watu walioko  katika hatari ya ukosefu wa fursa ili kuondokana na umasikini uliokithiri katiak nchi masikini.

FAO katika chapisho hilo la leo inasema mikakati hiyo inanufaisha watu takribani bilioni 2.1 katika nchi zinazoendelea kwa njia mbalimbali ikiwamo kuwakwamua watu milioni 150 dhidi ya umasikini uliokithiri. Benjamin Davis ni Kaimu Mkurugenzi wa FAO kitengo cha maendeleo ya uchumi wa kilimo.

(SAUTI ya Benjamin)

‘‘Ripoti inaonyesha kuwa ulinzi wa kijamii ni chombo fanisi katika kusaidia mahitji ya msingi ya maskini na wenye njaa na kusaidia ustawi wao. Mpango wa ulinzi wa kijamii ni muhimu katika kubadilisha maisha ya maskini na kuimarisha kilimo na jukumu la amaendeleo’"

Chapisho hilo limetolewa kuelekea siku ya chakula kimataifa mnamo Oktoba 16.