Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Katibu Mkuu apigia chepuo uwekezaji katika operesheni ya kulinda amani

Katibu Mkuu apigia chepuo uwekezaji katika operesheni ya kulinda amani

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amemshukuru Rais wa Baraza Kuu kwa kuandaa majadiliano ya jinsi ya kuboresha na kuimarisha operesheni ya amani ya umoja huo.

Akihutubia Baraza hilo, Ban amesema katika miaka ya karibuni kumekuwa na wasiwasi kuhusu kuenea kwa changamoto zinazokabili shughuli za Umoja wa Mataifa, ikiwa ni pamoja na kulinda amani na ujumbe maalum wa kisiasa.

Mwaka mmoja uliopita, Katibu Mkuu aliteua jopo maalum la kutathmini shughuli za amani ya Umoja wa Mataifa na kupendekeza jinsi ya kupambana na changamoto hizo.

"Operesheni za kulinda amani ni chombo cha kimataifa. Kuzifanya zifae kwa mahitaji yake, ni wajibu wetu sote. Kupitishwa kwa historia kwa malengo ya maendeleo endelevu mwezi uliopita, kunasisitiza ukweli wa muda mrefu: hakutakuwa na amani bila maendeleo; wala hakutakuwa na maendeleo bila amani, au kuheshimu haki za binadamu."