Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban alaani mfululizo wa mashambulizi Chad

Ban alaani mfululizo wa mashambulizi Chad

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani mfulululizo wa mashambulizi matano kutoka kwa kundi la kigaidi Boko Haram yaliyosababisha vifo nchini Chad mnamo Oktoba 10 ambapo watu kadhaa wamekufa na baadhi kujeruhiwa.

Taarifa ya Katibu Mkuu kupitia msemaji wake imemkariri Bwana Ban akituma salamu za rambirambi kwa waaathiriwa na serikali ya watu wa Chad.

Katibu Mkuu amepongeza Chad kwa kuchukua jukumu la kupambana na Boko Haram, pamoja na nchi za bonde la ziwa Chad kwa juhudi zao za pamoja katika kukabiliana na ugaidi . Ametaka mkutano uliokuwa umeahirishwa kati ya wakuu wa nchi za Afrika ya Kati na Magharibi kukutana hima kadri itakavyowezekana ili kukabiliana na ugaidi katika ukanda huo.

Mkutano wa viongozi hao uliahirishwa awali ambapo Ban amesema kufanyika kwake kutasaidia kuukaili ugaidi husuani katika kuangazia chanzo chake na kuheshimu sheria za kibinadamu , haki za binadamu na sheria za wakimbizi.