Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uvamizi wa Urusi kijeshi Syria usipuuzwe: Staffan de Mistura

Uvamizi wa Urusi kijeshi Syria usipuuzwe: Staffan de Mistura

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Syria Staffan de Mistura amesema hatua ya Urusi kuingilia kijeshi mgogoro nchini Syria imeibua mwenendo mpya ambao umesababisha haja ya kusaka suluhu ya kidiplomasia haraka kuliko wakati wowote.

Msuluhishi huyo wa mgogoro wa Syria ameonya kuendelea zaidi kwa mgogoro na kusisistiza kuwa mustakabli wa Syria hauwezi kuamuliwa kijeshi.

Ameongeza kuwa watu 40,000 wamekimbia katika maeneo ambapo kuna shughuli za majeshi yaliyovamia karibuni, idadi hiyo ikiongeza mzigo wakimbizi wa ndani milioni 1.2 baada ya miaka minne ya mapigano.

Bwana Staffan de Mistura amesema kuwa uvamizi wa kijeshi wa Urusi nchini Syria hauwezi kupuuzwa huku akisema kuwa suluhu ya kidiplomasia inasalia wazi kwa kuwa wadau wote wa kikanda na kimataifa wanafahamu kuwa mapema au badaye watafanay mazungumzo.