Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Haitawezekana kutimiza ajenda 2030 bila kutokomeza njaa hima- Ban

Haitawezekana kutimiza ajenda 2030 bila kutokomeza njaa hima- Ban

Ulimwengu hauwezi kutimiza ahadi ya ajenda ya maendeleo endelevu yam waka 2030 bila kufanya hima kutokomeza njaa na lishe duni.

Hayo ni kwa mujibu wa ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, ambao umesomwa na Mwakilishi wake maalum kuhusu uhakika wa kuwa na chakula na lishe, David Nabarro, wakati wa kikao cha 42 cha Kamati kuhusu

Uhakika wa kuwa na Chakula, CFS mjini Roma, Italia.

Ban amesema, baada ya kupitisha ajenda ya 2030 kuhusu maendeleo endelevu inayolenga kutokomeza umaskini, kuchagiza utajiri na maisha bora kwa wote, kulinda mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, kiungo muhimu kwa ufanisi wa ajenda hiyo ni kufikia uhakika wa kuwa na chakula, kuboresha lishe na kujenga mifumo ya dhabiti na jumuishi ya chakula.

Aidha, Ban amesema itakuwa vigumu kutimiza lengo la kutokomeza njaa na utapiamlo bila kutimiza malengo yote 17 ya maendeleo endelevu, akiongeza kuwa ajenda 2030 itahitaji mbinu mpya za utendaji kazi.