Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkataba wa tabianchi wa Paris ujumuishe suala la jinsia- UN Women

Mkataba wa tabianchi wa Paris ujumuishe suala la jinsia- UN Women

Msaidizi wa Katibu Mkuu na Naibu Mkuruigenzi Mtendaji wa Shirika linalohusika na masuala ya wanawake katika Umoja wa Mataifa, Radhika Coomaraswamy, amesema leo kuwa suala la jinsia na usawa linapaswa kuingizwa pia katika mkataba mpya kuhusu tabianchi mjini Paris, mwezi Disemba mwaka huu.

Bi Coomaraswamy amesema hayo leo wakati wa mkutano wa kamati ya Tatu ya Umoja wa Mataifa kuhusu kuendeleza hadhi ya wanawake.

Amesema ingawa hatua madhubuti zilipigwa katika mkutano wa kamati kuhusu hadhi ya wanawake, na ule viongozi wa kimataifa mnamo Septemba 27 2015 kuhusu usawa wa jinsia hivi karibuni, bado kuna hatua moja muhimu inayopaswa kupigwa ili kuendeleza hadhi ya wanawake hata zaidi.

(SAUTI ya COOMARASWAMY)

“Mabailiko ya tabianchi huathiri kwa njia tofauti wanawake na wanaume. Wanawake ni mawakala wa mabadiliko na viongozi katika kuhimili, kukabiliana na uthabiti. Mkataba huo ni lazima uwawezeshe wanawake kuongoza na kushiriki kikamilifu tunapokabiliana na athari za tabianchi pamoja.”