Skip to main content

Kutoka kuwa yaya hadi uongozi

Kutoka kuwa yaya hadi uongozi

Siku ya kimataifa ya mtoto wa kike ikiwa imeadhimishwa kote duniani mwishoni mwa wiki kwa jumbe wa kuwapa fursa wasichana ili wawe viongozi, nchini Tanzania maadhimisho hayo pamoja na mambo mengine yamejielekeza katika kuhamasisha jamii kuwa wasichana  waliokandamizwa wakiamua wanaweza.

Miongoni mwa wasichana ambaye alikuwa mfanyakazi wa kazi za ndani au yaya ambapo hivi sasa ni mwanaharakati mahiri nchini humo Anjela Mnagoza amesimulia ushuhuda wake wa namna alivyostawi katika mazingira magumu, na kuieleza hadhira wengi wao wakiwa wasichana kuwa

(SAUTI ya Anjela Mnagoza)

Kwenye ujumbe wake kwa siku hiyo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema ili kuwezesha watoto wa kike ni lazima kuwasaidia kuepukana na ndoa na mimba za utotoni, ukeketaji, na vile vile kuwapatia elimu bora na kuhakikisha wanakuwa na afya nzuri na ujuzi kuhusu haki zao katika maswala ya afya ya uzazi.