Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Teknolojia ya simu ya mkononi ya kupambana na TB

Teknolojia ya simu ya mkononi ya kupambana na TB

Shirika la Afya Duniani, WHO limetangaza mbinu mpya ya kupambana na kifua kikuu, au TB, kwa  kutumia simu ya mkononi na mtandao wa intaneti.

Chini ya mpango huo ulioko chini ya mapendekezo ya WHO na shirika la Ulaya la ugonjwa wa mapafu, serikali za kitaifa zitahamasishwa kutumia chombo hicho cha teknolojia kiitwacho suluhu ya afya ya dijitali, kutuma habari za kuokoa maisha kuhusu kifua kikuu kwa wafanyi kazi wa afya.

Dr Mario Raviglione wa WHO anaelezea, umuhimu wa teknolojia hiyo.

(SAUTI Dr Mario Raviglione)

"Kuwa na teknolojia ya intaneti ambayo itawafunza wauuguzi au kuwafundisha wale walio katika eneo la afya vijijini, katika pembezoni katika maeneo ya makazi duni kuwafundisha kutambua kifua kikuu, tayari ina manufaa kwa kutambua mapema ya kifua kikuu "