Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Katibu Mkuu alaani mashambulizi ya kigaidi Uturuki

Katibu Mkuu alaani mashambulizi ya kigaidi Uturuki

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani vikali mashambulizi ya kigaidi yaliyotokea leo mjini Ankara nchini Uturuki.

Taarifa iliyotolea leo na msemaji wake imesema kwamba makumi ya watu wamefariki kwenye shambulio hilo la kigaidi lililotokea wakati ambapo watu wakiandamana kwa amani, huku wengine zaidi ya 126 wakijeruhiwa.

Bwana Ban ameongeza kuwa anatarajia kwamba watekelezaji wa mashambulizi hayo watapelekwa mara moja mbele ya sheria.

Aidha ametuma salamu zake za rambirambi kwa familia za wahanga, pamoja na raia na serikali ya Uturuki, akiwatakia nafuu waliojeruhiwa.