Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Adhabu ya kifo haipaswi kutumiwa dhidi ya wafanyabiashara ya madawa ya kulevya: Ban

Adhabu ya kifo haipaswi kutumiwa dhidi ya wafanyabiashara ya madawa ya kulevya: Ban

Leo tarehe 10 mwezi Oktoba ikiwa ni siku ya kimataifa dhidi ya adhabu ya kifo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amepongeza hatua zilizochukuliwa na nchi nyingi duniani kote kutangua adhabu hiyo, akieleza kwamba miaka 70 iliyopita, nchi 14 tu zilizkuwa zimetangua adhabu ya kifo au kuacha kuitumia, zikiwa ni asilimia 82% sasa.

Katika ujumbe wake kwa siku hii, Katibu Mkuu amesema adhabu ya kifo ikitumiwa inapaswa kutekelezwa tu dhidi ya mauaji yenye nia ya kuua, wala si katika uhalifu mwingine kama vile biashara ya madawa ya kulevya.

Bwana Ban amekariri kuwa adhabu ya kifo haizuii uhalifu utokanao na madawa ya kulevya, wala haizuii watu kutumia madawa hayo.

Ameongeza kuwa ili kupunguza matumizi ya madawa ya kulevya, bora kubadilisha sekta ya sheria na kuwekeza katika huduma za afya na matibabu.

Hatimaye ametoa wito kwa serikali na watu binafsi kuendelea kupigania ili adhabu ya kifo iondolowe kabisa.