Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vurugu yaibuka Guinea kabla ya uchaguzi, Kamishna Zeid atoa wito wa utulivu

Vurugu yaibuka Guinea kabla ya uchaguzi, Kamishna Zeid atoa wito wa utulivu

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu Zeid Ra’ad Al Hussein ameeleza wasiwasi wake kuhusu hali ya ghasia iliyoibuka tangu Alhamis mjini Conakry, nchini Guinea.

Kwenye taarifa iliyotolewa leo na ofisi yake, Kamishna Zeid amesema vurugu na uporaji umetokea wakati ambapo raundi ya kwanza ya uchaguzi wa rais inatarajiwa kufanyika tarehe 11, Oktoba nchini humo.

Ameongeza kwamba vitendo hivyo vya ghasia vimetokea baada ya mapigano baina ya wafuasi wa chama tawala na wanachama wa vyama vya upinzani wiki iliyopita katika mji wa N’Zerekore, kusini mwa nchi, ambapo zaidi ya watu 45 wamejeruhiwa.

Kamishna Zeid amewasihi viongozi wa kisiasa kujitahidi kushawishi wafuasi wao watulie na kusitisha vurugu hizo.