Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali ya walimu Afrika Mashariki

Hali ya walimu Afrika Mashariki

Wakati ambapo jamii ya kimataifa imeadhimisha siku ya walimu duniani, hapo tarehe 5, Oktoba, Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni UNESCO limekariri wito wake wa kuhakikisha kwamba walimu wanaajiriwa wa kutosha na wanawezeshwa ili kuwapatia watoto wote duniani elimu bora.

Ili kutimiza lengo hili UNESCO imependekeza  kuwa idadi ya wanafunzi wanaosomeshwa darasani na mwalimu mmoja isizidi 40. Kwa hiyo imekadiria kuwa itabidi kuajiri walimu milioni 6 ifikapo 2030, pamoja na kuwapatia mafunzo wanaostahili.

Je Hali Tanzania iko je? Priscilla Lecomte ameongea na Tumsifu Mmari, Mkuu wa sekta ya elimu ya UNESCO.