Serikali ya Umoja wa Kitaifa yaundwa nchini Libya
Baada ya mwaka mmoja wa mashauriano na mazungumzo na washikadau mbali mbali nchini Libya hatimaye tangazo la kuundwa kwa serikali ya Umoja w akitaifa limetolewa leo. Taarifa kamili na Priscillla Lecomte
(TAARIFA YA PRISCILLA)
Nats!
(Finally, the moment has come in which we can propose the unity government)
Ni mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Libya, Bernadino Leon, akitangaza kuundwa kwa serikali ya Umoja wa Kitaifa nchini humo. Anasema hatimaye wakati umewadia ambapo twaweza kupendekeza serikali ya Umoja wa kataifa.
Akizungumza na waandishi wa habari kutoka mji wa Skhirat nchini Morocco, Leon amesema Walibya Wengi wamepoteza maisha yao, watoto na wanawake wameteseka, na kwa mujibu wa mashairka ya Umoja wa Mataifa karibu Walibya milioni 2.4 wanamahitaji ya kibinadamu.
Kwa mujibu wa kiongozi huyo, Serikali hiyo itakuwa na wajumbe sita wa Baraza la Rais, ikimjumuisha Waziri Mkuu Fayez Sarraj , Mbunge kutoka Tripoli, Naibu Waziri Mkuu, anayewakilisha magharibi , mashariki na kusini mwa nchi hiyo, kwa mtiririko huo; na Mawaziri wawili waandamizi.
Kwa maantiki hiyo, Leon ameomba radhi kwa kutopendekeza serikali hii mapema, lakini akaongeza pia ni furaha kwa sababu angalau kuna nafasi ya kuitangaza.
(SAUTI LEON)
“Hii haikuwa kazi rahisi. Tumekuwa tukisikiliza watu wengi ndani na nje ya mazungumzo. Na tunaamini kwamba orodha hii ni nzuri. Lakini kama nilivyosema, tunahamasisha watu wa Libya kuelewa kwamba chaguzi haukuwa usio na mipaka, na kwa hiyo ukamilifu labda usingewezekana”