Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tuzo ya amani ya Nobel yaenda Tunisia, Ban apongeza

Tuzo ya amani ya Nobel yaenda Tunisia, Ban apongeza

Tuzo ya amani ya Nobel kwa mwaka huu wa 2015 imekwenda kwa kikundi kilichoongoza maridhiano ya kitaifa nchini Tunisia baada ya vuguvugu la kisiasa la mwaka 2011.

Pande nne zilishiriki kwenye mazungumzo hayo ambazo ni chama cha wafanyakazi Tunisia, shirikisho la viwanda Tunisia, chama cha haki za binadamu Tunisia na kikundi cha wanasheria nchini humo.

Kufuatia ushindi huo, Katibu Mkuu ametuma pongezi akisema ushindi huo ni kwa wananchi wote wa Tunisia ambao walichagiza vuguvugu la nchi za kiarabu ambalo hata hivyo licha ya kupoteza maisha ya raia bado walilinda kile walichotetea na kuleta mabadiliko.

Ban amesema Umoja wa Mataifa utaendelea kusimama kidete na kwa mshikamano na washindi wa tuzo hiyo ya amani ya Nobel wanaposonga mbele kujenga taifa lenye amani na demokrasia ambayo wananchi wote wana haki nayo.