Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban amteua Maman Sidikou kuwa mkuu wa MONUSCO

Ban amteua Maman Sidikou kuwa mkuu wa MONUSCO

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon, ametangaza leo kuteuliwa kwa Maman Sambo Sidikou wa Niger kuwa Mwakilishi wake maalum nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo, MONUSCO.

Bwana Sidikou anairithi nafasi ya Martin Kobler wa Ujerumani, ambaye Katibu Mkuu amemshukuru kwa mchango wake mkubwa na utumishi wa kujituma kwa miaka miwili iliyopita, katika kusaidia kutekeleza mamlaka ya MONUSCO.

Bwana Sidikou ambaye sasa ni Mwakilishi maalum wa AU nchini Somalia na Mkuu wa ujumbe wa AU, AMISOM, ana uzoefu mkubwa, akiwa amehudumu katika nyadhfa mbalimbali nchini mwake na kimataifa, kwenye Umoja wa Mataifa na kama afisa wa ngazi ya juu katika Muungano wa Afrika, AU.

Sidikou pia alikuwa balozi wa Niger Marekani kati ya 2011 na 2014.