Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakimbizi wa Afghanistan wasisahauliwe

Wakimbizi wa Afghanistan wasisahauliwe

Jumuiya ya kimataifa leo imesaini ahadi ya kutafutia ufumbuzi wa kudumu kwa tatizo la mamilioni ya wakimbizi wa Afghanistan, katika jitihada za kumaliza mojawapo ya hali ya kuachwa bila makao ya muda mrefu katika historia.

Katika taarifa iliyotolewa wakati wa mkutano wa 66 wa Kamati ya Utendaji ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR, nchi wanachama zimeahidi msaada kwa Afghanistan ili kujenga mazingira muhimu kwa wakimbizi wa Afghanistan kurejea nyumbani na kujumuika katika jamii.

Kamishna Mkuu wa Shirika la kuhudumia Wakimbizi , UNHCR Antonio Guterres, amesema kupuuza Afghanistan itakuwa hatari, bila kujali umuhimu na ukubwa wa migogoro mingine mapya.

Halikadhalika, Guterres amesema kutoka mtazamo wa kukabiliana na maswala ya kibinadamu, ni wazi kwamba, hatua kwa hatua kutatua migogoro ya zamani ni muhimu kabisa ili kuepuka kuzidiwa kabisa na janga mpya.