Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tutaweza kutangaza serikali ya umoja wa kitaifa Leo: Leon

Tutaweza kutangaza serikali ya umoja wa kitaifa Leo: Leon

Juhudi za kutafutia ufumbuzi mgogoro wa Libya zimeimarishwa, baada ya Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Libya, Bernadino Leon, kusema kuwa badala ya kutangaza serikali ya Kitaifa kama ilivyoyotarajiwa, wajumbe katika mchakato wa  mazungumzo ya kitaifa wamekubaliana kuendelea na kazi hadi kesho ambapo tangazo kuhusu kuundwa kwa serikali hiyo ya kitaifa litakapotolewa.

Tangazo hilo litakuwa hatua muhimu ya kisiasa katika kuleta amani nchini Libya.

Akizungumza na waandishi wa habari kutoka mji mwa Skhirat, nchini Morocco ambapo mazungumzo yanaedelea, Leon amesema, hakuna vikwazo vitakavyozuia mjadala wa kitaifa kupendekeza serikali ya umoja wa kitaifa- serikali imara ambayo itawaunganisha Walibya wote na kuwaruhusu kukabiliana na mzozo wa kiusalama, na wa kibinadamu unaowakabili.

(SAUTI LEON)

"Kwa hiyo ujumbe usiku wa leo ni ujumbe wa umoja . Ni ujumbe wa uaminifu. Tunajua vizuri kwamba kuna Walibya wengi ambao wamechanganyikiwa baada ya kile kilichotokea leo.  Ningependa kusema kwamba baada ya kushauriana na watu wengi ndani na nje ya Tripoli, Libya, nawaambia kwamba sisi tutashinda, na kwamba tutapendekeza serikali kesho”