Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tanzania na maadhimisho ya miaka 70 ya UM

Tanzania na maadhimisho ya miaka 70 ya UM

Nchini Tanzania kumefanyika mkutano wa uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa ambapo mratibu mkazi wa Umoja huo nchini humo Alvaro Rodriguez amezungumzia umuhimu wa kutunza amani ili malengo ya maendeleo endelevu yaweze kutekelezeka.

Mkutano huo ulihudhuriwa pia na Kaimu Katibu Mkuu wa izara ya Mambo ya Nje na ushirikiano wa kimataifa Balozi Hassan Simba Yahaya ambaye alitumia fursa hiyo kusema kuwa Tanzania imejiandaa vyema kutekeleza malengo hayo huku akisema..

(Sauti ya Balozi Yahya)

Kilele cha maadhimisho hayo ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania kitakuwa tarehe 13 mwezi huu jijini Dar es salaam.