Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bidhaa kuanza kushuka: FAO

Bidhaa kuanza kushuka: FAO

Bidhaa za kilimo zinashuka bei lakini pia haizitabiriki limesema shirika la chakula na kilimo FAO.

Katika taarifa yake FAO imesema baada ya kipindi kirefu cha kupanda kwa bei tangu mwaka 2007 hadi mapema 2011, bei za nafaka na mafuta ya mboga ziko katika mwelekeo wa kutopanda na kushuka.

Taarifa hiyo inataja sababu za kushuka kwa bei kuwa ni pamoja na viwango vya hesabu, kushuka kwa bei za mafuta na uimara wa dola ya Kimarekani. Sababu nyingine ambayo FAO imesema haiwezi kuwekwa kando ni hali ya hewa inayoweza kuathiri mavuno.

Watalaamu wa bidhaa kutoka FAO wakifafanua amesema kuwa ujumbe muhimu ni kwamba kitakwimu, mabadiliko ya hivi karibuni katika bidhaa yanatabiri kushuka kwa bei na hali ya kutotabirika.