Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wiki nzima bila kisa cha Ebola Afrika Magharibi: WHO

Wiki nzima bila kisa cha Ebola Afrika Magharibi: WHO

Hatua kwa hatua, kuna nuru katika jitihada za kutokomeza kabisa homa ya Ebola huko Afrika Magahribi baada ya mataifa matatu yaliyoathiriwa zaidi na ugonjwa huo kutoripoti kisa chochote kipya kwa wiki moja sasa. Taarifa zaidi na Assumpta Massoi.

(Taarifa ya Assumpta)

Maafisa wa shirika la afya duniani, WHO wamesema nchi hizo Liberia, Sierra Leone na Guinea ambazo hazijaripoti kisa chochote kwa wiki moja sasa na hii ni mara ya kwanza tangu mwezi Machi mwaka jana, Ebola ilipolipuka Afrika Magharibi.

Liberia ilitangazwa kuwa huru kutokana na maambukizi ya Ebola mwanzoni mwa mwezi Septemba, Sierra Leone haijawahi kuwa na kisa kilichothibitishwa cha homa hiyo kali kwa muda wa wiki tatu sasa, huku nchini Guinea, hakuna kisa chochote kwa muda wa wiki moja.

Hata hivyo, WHO imeonya, japo hali hii ni habari njema, bado kuna hatari kubwa ya maambukizi hivyo ni vyema kuendelea kuwa makini.