Nchi za Afrika zajinasibu na nishati ya nyuklia, Kenya iko mbioni
Zaidi ya nchi 30 duniani, theluthi moja zikitoka Afrika zinajiandaa kuanzisha mipango ya nyuklia kwa ajili ya kuzalisha umeme kwa usaidizi wa utalaamu kutoka shirika la nishati ya atomiki duniani, IAEA.
Hatua hiyo inatoana na uhaba wa nishati kupitia mbinu za sasa za uzalishaji umeme ikiwemo maji ambapo mwenyekiti mtendaji wa bodi ya umeme wa nyuklia nchini humo Ochilo Ayacko amesema hadi mwaka 2030 wanahitaji GhW 19 ili kufikia ukuaji uchumi wanaohitaji na hivyo..
(Sauti ya Ochilo)
“Ili kufanya hivyo, tumeangalia mbinu tofauti za uzalishaji umeme. Tumekuwa tunachanganya vyanzo vya gesi, makaa ya mawe, kutumia joto la ardhini, na sasa tunahitaji nyuklia. Ni kwamba tunahitaji vyanzo vingi na tofauti vya kuzalisha umeme ili kuwa na uhakika wa nishati nchini Kenya.”
IAEA imesisitiza kuwa jukumu lake ni kusaidia nchi ambazo zina mpango wa kutumia nyuklia kama chanzo salama, cha uhakika na rahisi cha nishati lakini ni uamuzi wa nchi husika kuamua iwapo nishati hiyo ni sahihi kwake au la.
Ripoti ya IAEA inaonyesha kuwa ni theluthi moja tu ya wakazi wa nchi za Afrika zilizo kusini mwa jangwa la Sahara ndio wanaopata umeme.