Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watoto CAR wanakosa elimu kutokana na machafuko- OCHA

Watoto CAR wanakosa elimu kutokana na machafuko- OCHA

Mashirika ya kibinadamu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, yanakadiria kuwa takriban watoto 15,600 mjini Bangui hapati elimu, kutokana na watu kulazimika kuhama hivi karibuni na machafuko.

Kwa mujibu wa taarifa ya Ofisi ya kuratibu masuala ya kibinadamu, OCHA, muhula wa kwanza wa mwaka mpya wa shule ulianza mnamo Septemba 21, lakini shule nyingi badi zimefungwa kwa sababu ya kuibuka machafuko hivi karibuni.

Shule ambazo zimefunguliwa zinakabiliwa na tishio la mashambulizi, na hivyo kuhatarisha usalama wa wanafunzi na walimu.

Kuna pia ripoti za kufurushwa upya kwa watu kati ya 8,000 na 10,000 katika mkoa wa Kemo, eneo la kati mwa nchi, kufuatia machafuko ya Oktoba 2, 2015. Wengi wa waliolazimika kuhama wamekimbilia parokia ya kanisa katoliki karibu na kituo cha ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kuweka utulivu nchini humo, MINUSCA.