Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yapata kibali cha kambi tatu mpya nchini Tanzania

UNHCR yapata kibali cha kambi tatu mpya nchini Tanzania

Nchini Tanzania, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR leo limeanza kuwahamisha wakimbizi Elfu 50 kutoka kambi ya Nyarugusu mkoani Kigoma kwenda kambi nyingine mbili za mkoa huo uliopo kaskazini magharibi mwa nchi hiyo.

Katika tovuti yake, UNHCR imesema kambi hizo za Nduta na Mtendeli zitasaidia kupunguza msongamano katika kambi ya Nyarugusu ambayo inaelezwa kuwa ni kambi kubwa zaidi na yenye msongamano zaidi duniani.

UNHCR imesema hatua hii inafuatia mashauriano kadhaa ikiwemo kati ya Kamishna Mkuu wa UNHCR Antonio Guterres na Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania huko Geneva, Uswisi miezi micheche iliyopita na kwamba serikali ya Tanzania imewapatia vibali vya kutumia kambi hizo mbili pamoja na ile ya Karago ambayo itafunguliwa mwakani baada ya kurekebisha miundombinu yake ya maji.

Mpango wa uhamishaji unahusisha wakimbizi kusafirishwa kwa barabara ambapo awamu ya kwanza ni wakimbizi wapya na wale walio katika mazingira magumu zaidi.