Skip to main content

UNCDF kuimarisha serikali za mitaa Uganda

UNCDF kuimarisha serikali za mitaa Uganda

Nchini Uganda, Mfuko wa Maendeleo ya Mitaji wa Umoja wa Mataifa(UNCDF) umezindua leo mradi wa zaidi ya dola milioni 2.6 wa kuwezesha serikali za mitaa kuimarisha miundombinu kupitia ushirikiano na sekta binafsi na wizara ya serikali za mitaa.

Uzinduzi huo umefanyika kwenye mkutano wa siku mbili ulioanza leo mjini Kampala, nchini Uganda kwa ajili ya kuzungumzia mifano bora ya uwekezaji katika ngazi ya mitaa.

Peter Malika  mshauri mkuu wa UNCDF kuhusu maswala hayo amesema mradi huo unalenga kufadhili miradi ya kujenga miundumbinu kama vile za usafiri, umwagiliaji maji, uzalishaji wa nishati, viwanda vya vyakula, ghala au masoko.

(Sauti ya Peter Malika)