Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kazi ya MONUSCO bado haijakamilika DRC:Kobler

Kazi ya MONUSCO bado haijakamilika DRC:Kobler

Bado lengo la Ujumbe wa Umoja wa Mataifa MONUSCO halijatimizwa, amesema leo mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC Martin Kobler, akiwasilisha ripoti ya Katibu Mkuu mbele ya Baraza la Usalama. Taarifa zaidi na Grace Kaneyia.

(Taarifa ya Grace)

Akihutubia wanachama wa Baraza la Usalama kwa mara ya mwisho baada ya kuhudumu DRC kwa zaidi ya miaka miwili, bwana Kobler amesema uchaguzi utakaofanyika mwaka kesho nchini humo tayari unachochea mvutano na ghasia, akieleza wasiwasi wake juu ya visa 2,200 vya ukiukaji wa haki za binadamu vilivyotokea mwaka huu na kutoa wito kwa viongozi.

(Sauti ya Kobler)

Aidha amesema kuimarishwa kwa ufanisi wa MONUSCO pamoja na operesheni za pamoja na jeshi la kitaifa la FARDC kumechangia kurejeshwa kwa usalama kwenye baadhi ya maeneo mashariki mwa nchi.

Hata hivyo bwana Kobler amesisitiza kwamba mamilioni ya wacongo wanateseka na janga la vita kutokana na uhalifu unaofanywa na waasi wa FDLR na ADF.

(Sauti ya Kobler)

Hatimaye akimulika umuhimu kwa MONUSCO kuondoka nchini humo, amesema utaratibu huo unaopaswa kufanywa taratibu kwa ushirikiano na FARDC.