Marekani yasaidia WFP Uganda

6 Oktoba 2015

Marekani kupitia shirika lake la Maendeelo ya Kimataifa (USAID),imetoa dola Milioni tisa kwa ajili ya kuwezesha Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP), kushughulikia mahitaji ya  chakula kwa maelfu ya wakimbizi nchini Uganda. Taarifa kamili na John Kibego.

(Taarifa ya John Kibego)

Mchango huo umepokewa kwa mikono miwili wakati WFP ilikuwa inakaribia kukata mgao wa chakula hata kwa wakimbizi wapya wanaomiminika kutoka Sudan Kusini.

Hii ni kwa mujibu wa Michael Dunford Mkurugenzi wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) humo nchini.

Bwana Dunford amesema fedha hizo zitatumiwa kununua tani 13,000 za nafaka na maharagwe za kulisha zaidi ya wakimbizi laki tatu.

Kwa sasa idadi ya wakimbizi humo nchini ni karibu nusu milioni, wengi wakiwa wametoka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Sudan Kusini na Burundi.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud