Skip to main content

Hali CAR yaimarika licha ya mvutano

Hali CAR yaimarika licha ya mvutano

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, MINUSCA umesema hali ya usalama kwenye mji mkuu Bangui, inaimarika licha ya mvutano unaoendelea.

Hii ni kwa mujibu wa msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric aliyeongea na waandishi wa habari leo mjini New York Marekani akisema maduka yameanza tena kufunguliwa na magari kutembea tena barabarani, huku wanajeshi wa MINUSCA na askari wa Ufaransa Sangaris wakifanya doria mjini humo mwishoni mwa wiki.

Bwana Dujarric amesema MINUSCA imeondoa vizuizi vyote vilivyokuwepo barabarani mjini Bangui, ikishirikiana na Sangaris ili kuzuia waasi waliokuwa wa Seleka kusafiri kusini mwa eneo hilo.

Aidha ameeleza kwamba mwishoni mwa wiki iliyopita, pia MINUSCA imelazimika kujibu mashambulizi kwa wanamgambo waliokuwa wanafyatulia risasi askari wanaolinda ofisi za Umoja wa Mataifa mjini Bangui.