Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kushuka kwa bei ya Bidhaa dunaini , vikwazo vya umeme na ukosefu wa Usalama yapunguza ukuwaji wa Uchumi Afrika: Benki ya dunia

Kushuka kwa bei ya Bidhaa dunaini , vikwazo vya umeme na ukosefu wa Usalama yapunguza ukuwaji wa Uchumi Afrika: Benki ya dunia

Kadri mazingira magumu ya kiuchumi ya kimataifa yanavyozidi kujiri, pamoja na changamoto za kitaifa zinavyozidi kukabili nchi nyingi za kiafrika, ndivyo ukuaji wa kiuchumi Afrika kusini mwa jangwa la Sahara utaendelea kuwa hafifu. Taarifa zaidi na Abdullahi Boru.

(Taarifa ya Abdullahi)

Hiyo ni kwa mujibu wa Benki ya dunia ikisema makadirio yake mapya kwa mwaka huu wa 2015, ukuaji wa kiuchumi utapungua na kufikia asilimia 3.7 kinyume na asilimia 4.6 mwaka uliopita.

Tathmini ya ripoti mpya ya benki hiyo inasema, hali hiyo imetokana na kushuka kwa bei za bidhaa muhimu mathalan mafuta, shaba na chuma, sawia na kushuka kwa uchumi wa China, na kudorora kwa hali ya fedha duniani.

Ukuaji huo wa kiuchumi wa 2015 ni kiwango cha chini kwa mataifa ya Kiafrika yaliyo Kusini mwa Jangwa la Sahara tangu mwaka 2009, na iko chini ya ukuaji imara wa kila mwaka wa asilimia 6.5. kwa eneo hilo tangu mwaka wa 2003-2008.

Hata hivyo, Punam Chuhan - Pole , Kaimu Mwanauchumi Mkuu wa Benki ya Dunia Ukanda wa Afrika amesema , habari njema ni kwamba mahitaji ya ndani yanayotokana na matumizi , uwekezaji, na matumizi ya serikali vitachochea ukuaji wa uchumi kwa asilimia zaidi ya 4.4 mwaka 2016, na kufikia asilimia 4.8 mwaka 2017.