Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Usalama, amani na maendeleo ni kielelezo cha mchango wa UM Malawi: Rais Mutharika

Usalama, amani na maendeleo ni kielelezo cha mchango wa UM Malawi: Rais Mutharika

Umoja wa Mataifa una mchango mkubwa katika usalama na amani nchini Malawi na ukanda huo amaesema Rais wa nchi hiyo Profesa Peter Mutharika katika mahojiano maalum na idhaa hii mjini New York amezungumizia mchango wa chombo hicho kinachoadhimisha miaka 70 tangu kuasisiwa.

Rais Mutharika amesema matahalani katika ulinzi wa amani nchi yake iko mstari wa mbele kusaidia nchi zenye migogoro zoezi linaloratibiwa na Umoja huo.

(SAUTI MUTHARIKA )

‘‘Umoja wa Mataifa unachangia vya kutosha katika usalama, kwa mfano tuna vikosi vya kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC tukishirikiana na Tanzania na Afrika Kusini. Kwa mara ya kwanza kabisa kamanda wa vikosi hivyo anatoka Malawi. Vikosi vyetu pia viko Darfur, Cote d’ lvoire.’’