Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Walimu milioni 6 wahitajika barani Afrika ifikapo 2030

Walimu milioni 6 wahitajika barani Afrika ifikapo 2030

Leo ikiwa ni siku ya walimu duniani, Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni UNESCO linamulika mzozo wa walimu barani Afrika, likisema walimu zaidi ya milioni 6 watahitajika barani humo ifikapo mwaka 2030 ili kuwapatia watoto wote elimu bora. Taarifa kamili na Priscilla Lecomte

(Taarifa ya Priscilla)

Kwenye taarifa iliyotolewa leo, UNESCO imesema walimu zaidi wanahitajika kwa sababu idadi ya watoto inazidi kuongezeka. Tayari walimu milioni 2.7 wanahitajika sasa hivi ili kufika uwiano unaopendekezwa na UNESCO wa mwalimu mmoja kwa wanafunzi 40, pamoja na kuwafikia watoto karibu milioni 60 ambao hawakuandikishwa shuleni.

Maudhui ya mwaka huu yakiwa ni: kuwezesha walimu kwa ajili ya kujenga jamii endelevu, UNESCO imesisitiza umuhimu wa masomo ya walimu, ikisema changamoto ya uhaba wa walimu ni kuwa wengi wao wanaajiriwa bila kufundishwa ipasavyo.

Katibu mtendaji wa tume ya taifa ya UNECSO nchini Tanzania Dkt. Moshi Kiminzi anatoa wito wa umuhimu wa walimu.

(Sauti ya Dkt. Kiminzi)