Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kwenye Siku ya Makazi Duniani, maeneo bora ya umma yapigiwa chepuo

Kwenye Siku ya Makazi Duniani, maeneo bora ya umma yapigiwa chepuo

Ikiwa leo ni Siku ya Makazi Duniani, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon, amesema maeneo ya umma ni muhimu kwa watu walio hatarini, akiongeza kwamba kuwawezesha watu kuyafikia na kuyafanya yawe salama kwa wanawake na wasichana, kunaongeza usawa, kunaendeleza ujumuishaji na kupambana na ubaguzi.

Kauli mbiu ya maadhimisho ya siku hii mwaka huu ni “maeneo ya umma kwa wote”, ikishirikisha kampeni ya #He4She ya kuendeleza usawa wa jinsia. Katika ujumbe wake, Katibu Mkuu Ban Ki-moon amesema maeneo bora ya umma huwawezesha watu kuwasiliana na kujumuika na wenzao, na kushiriki katika maisha ya umma.

Katika ujumbe wake wa siku hii, Mkuregenzi Mtendaji wa Shirika la Makazi la Umoja wa Mataifa, UN Habitat, Juan Clos, amesema ubora wa maisha ya watu mijini una uhusiano wa moja kwa moja na hali maeneo ya umma.

Maeneo ya umma hutoa fursa ya mwingiliano wa kijamii na kitamaduni, na yanaweza kuendeleza hisia za uwenyeji na fahari mahali popote pale. Maeneo ya wazi yaliyo wazi kwa wote, bila kujali asili ya kabila, umri au jinsia, hutoa jukwaa la kidemokrasia kwa raia na jamii.”