Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Majanga ya kibinadamu hayawezi kumalizwa kibinadamu:Guterres

Majanga ya kibinadamu hayawezi kumalizwa kibinadamu:Guterres

Kamishna Mkuu wa shirika la kuhudumia wakimbizi duniani, UNHCR Antonio Guterres amefungua kikao cha 66 cha kamati tendaji ya shirika hilo huko  Geneva na kusema kuwa hakuna suluhu la kibinadamu kwenye majanga ya kibinadamu yanayosababishwa na mizozo. Taarifa zaidi na Joshua Mmali.

(Taarifa ya Joshua)

Guterres amesema suluhu pekee ni la kisiasa katika mizozo hiyo lakini kinachokosekana sasa kufanikisha hilo kwenye mizozo mikubwa inayoendelea sasa duniani ni dalali wa dhati kwenye mijadala na uwezo wa kuziweka meza moja nchi ambazo zinachochea mapigano.

Hivyo amesema..

(Sauti ya Guterres)

“Hatutashuhudia mabadiliko ya dhati hadi pale serikali zinazofadhili fedha na silaha kwa pande za mizozo inayoendelea, zitakapomaliza tofauti zao na maslahi ya kimizozo na kutambua kuwa kila upande unashindwa kwenye vita hivyo na kukubaliana mwelekeo mmoja wa kumaliza umwagaji damu.”

Kuhusu wahamiaji na wakimbizi kutoka Afrika, wanaokwenda Ulaya kusaka maisha bora au kuokoa maisha yao, Guterres amesema mkutano ujao wa Malta katiya Afrika na Ulaya kuhusu uhamiaji utakuwa ni fursa ya kuweka sera mpya za ushirikiano zitakazozingatia uhamiaji.